Hub for education news and events

Bajeti elimu ya bure yaongezwa kutoka Bilioni. 18 hadi 22 kwa mwezi

Serikali imeongeza bajeti katika elimu ya bure kutoka Sh bilioni 18 hadi Billioni 22 kwa mwezi, imefanya hivyo ili iweze kutekelezaji wa sera ya elimu bure kwa ngazi ya elimu ya msingi hadi sekondari kidato cha sita.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Elimu ya bure imeanzishwa Januari mwaka jana na serikali ya awamu ya tano ambapo kwa kuanza serikali ilikuwa inatoa Sh. bilioni 18.77 kila mwezi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivi karibumu alikaririwa akisema kuwa serikali inatoa Sh. bilioni 22 kila mwezi kwa ajili ya kuzigawa katika shule zote kutumika kwa shughuli za kiutendaji, Waziri Mkuu alikuwa akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mji mdogo wa Mlowo, Halmashauri ya Mbozi mkoani Songwe. 

Waziri Mkuu alisema kutokana na kutoa kiasi hicho cha fedha, hategemei kusikia walimu wakichangisha wanafunzi michango yoyote kwa ajili ya elimu.

“Tulianza na madawati, tukaja mifumo mashuleni na sasa tumetoa michango, lengo tunataka kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule ahakikishe anasoma bila kubughudhiwa, ikibainika shule yoyote inayotoza, basi watendaji wake ajiandae kutumbuliwa.”

Wananchi waliuliza maswali ambapo Waziri Mkuu alisaidiwa kujibu maswali hayo na wakuu wa idara alijibu kutokana na swali lenyewe, mwisho walifanya tathimini ya ziara ya siku nne ambayo ilimalizika jana.

Add a comment (0)

Vyuo 19 vyafungungiwa kufanya udahili 2017/2018

Tume  ya  Vyuo  Vikuu  Tanzania  (TCU) imesema imevisimamisha vyuo 19 nchini visifanye udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/2018 kwa sababu havina sifa.

Taarifa ilitolewa hivi karibuni imesema tume hiyo ilifanya uhakiki wa vyuo Sept na Oct mwaka jana na kubaini vyuo hivyo havina sifa ya kudalii hivyo imevisimamisha hadi hapo uamuzi utakapo tangazwa vinginevyo.

"Ripoti  ya  uhakiki  ilionesha  mapungufu  kadhaa  katika  baadhi  vyuo.  Kwa sababu  hiyo,
Tume  imesitisha udahili wa wanafunzi  wa  mwaka  wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18" ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilivitaja vyuo hivyo kuwa ni;-

1. Eckenforde Tanga University
2. Jomo Kenyatta University, Arusha
3. Kenyatta University, Arusha
4. United African University of Tanzania
5. International Medical and Technological University (IMTU)
6. University of Bagamoyo
7. St. Francis U niversity College of Health and Allied Sciences
8. Archibishop James University College
9. Archibishop Mihayo University College
10. Cardinal Rugambwa Memorial University College
11. Kampala International University Dsm College
12. Marian University College
13. St. Johns Univer sity of Tanzania Msalato Centre
14. St. Johns University of Tanzania, Marks Centre
15. St. Joseph University College of Engineering and Technology
16. Teofilo Kisanji University
17. Teofilo Kisanji University Tabora Centre
18. Tumaini University, Mbeya Centre
19. Kilimanjaro Chri stian Medical University College (KCMCo)

Aidha katika taarifa hiyo, ilisema kutokana na  mapungufu  katika  vyuo  mbalimbali
tume imeamua kwamba  jumla  ya  programu 75 kutoka  vyuo  22 nchini  zimesitishwa
kudahili  wanafunzi  mwaka  wa  masomo  2017/18.

Programu ambazo zimesitishwa kudahili wanafunzi bonyeza hapa

Vile vile tume  inapenda  kusisitiza  kwamba,  uamuzi  huu  hautawahusu
wanafunzi wanaondelea na masomo katika programu na vyuo husika.

Add a comment (0)

Wanafunzi kutumia namba moja kuzuia wanafunzi hewa

Kuanzishwa kwa mfumo wa namba maalumu ya usajili itakayotumiwa na wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi chuo ngazi ya diploma, kutasaidia kupunguza tatizo la wanafunzi hewa.
Hayo yalitangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mitihani wa Necta, Khalifan Kabiki alisema utaratibu huo unafuta uliokuwa unatumika zamani ambapo mwanafunzi alipewa namba mpya kila alipofanya mtihani.


Mfumo mpya, utamtambua mwanafunzi kwa namba atakayosajiliwa nayo darasa la kwanza ambayo ataitumia katika maisha yake yote ya shule na taarifa zake zote zitakuwa humo.

Kabiki alisema mfumo huo ambao utakuwa wa kielektroniki, utasaidia uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa kutoa namba maalumu itakayomtambulisha mwanafunzi katika ngazi mbalimbali za mafunzo.

“Mfumo huu utasadia katika uandaaji na utoaji wa takwimu za wanafunzi katika ngazi ya shule, wilaya, mkoa na Taifa. Pia utarahisisha ufuatiliaji wa taarifa za matokeo ya kila mwanafunzi ili kuhakikisha wadau wa elimu wanapata ufahamu wa kutosha kuhusu ufundishaji na ujifunzaji,” alisema Kabiki.

Pia, mfumo huo utasaidia katika uhamisho wa mwanafunzi ndani na nje ya mkoa, kwani namba hiyo itakuwa ina taarifa zake zote muhimu na hakutakuwa na haja ya vielelezo vingine.

Kabiki alisema tayari mfumo huo umeanza kujaribiwa katika mikoa ya Mwanza na Ruvuma, na ifikapo Desemba utaimarishwa zaidi ili kuanzia Januari uanze kutumika nchi nzima.

Katika hatua nyingine, ofisa habari wa baraza hilo, John Nchimbi alisema Necta imeboresha mfumo wa usahihishaji mitihani ya Taifa kwa kuweka wasahihishaji kulingana na idadi ya maswali kwa kila somo.

Pia, Necta walisema wameimarisha udhibiti wa wizi wa mitihani na udanganyifu kwa kipindi cha miaka minne, kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.

“Usahihishaji wa sasa unatumia mfumo wa mnyororo kuepuka baadhi ya wasahihishaji kumkosesha mwanafunzi swali ambalo amelijibu kwa ufasaha kwa kuwa tu maswali yaliyotangulia alikuwa hajayajibu vizuri,” alisema.

Alisema mfumo wa kudhibiti wizi wa mitihani na udanganyifu umeimarishwa kutoka watahiniwa wadanganyifu 9,736 mwaka 2011 mpaka sifuri mwaka 2015 kwa elimu ya msingi. Kwa kidato cha nne wanafunzi 3,303 walifanya wizi na udanganyifu huo kwa mwaka 2011 lakini idadi hiyo imepungua mpaka wanafunzi 87 mwaka 2015.

Nchimbi alisema mfumo huo umepunguza wizi na udanganyifu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kutoka 11 mwaka 2011 mpaka tano mwaka 2015.

Chanzo Mwananchi

Add a comment (0)

Kenya serikali kutoa huduma ya Internet kwa sekondari 1000

MAMLAKA ya mawasiliano Nchini (CA) inapanga kuweka Intaneti (broadband internet) katika shule 1000 za sekondari za umma nchini kwa gharama ya Sh500 milioni ili kurahisisha masomo kupitia mtandao (online learning). Mradi huo utafaidi shule amabazo zina maabara, kompyuta zinazofanya kazi na vifaa vingine vya teknolojia ya habari (IT).

Akizungumza Jumamosi katika shule ya mseto ya kutwa ya Mulathakari Kaunti ya Meru wakati wa harambee ya kuchangisha pesa ya kujenga ukumbi makuli, Mkurugenzi Mkuu wa CA Bw Francis Wangusi alisema kuwa wanachagua shule ambazo zinaweza kurahisisha mradi huo.

Add a comment (0)

Read more: Kenya serikali kutoa huduma ya Internet kwa sekondari 1000

Benki ya Walimu yaanza kuuza hisa.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Tamisemi (Elimu), Kassim Majaliwa (pichani), jana alizindua uuzwaji wa hisa za Benki tarajiwa ya Walimu (MCB) na kuutaka uongozi wake kutoruhusu ubadhirifu ili kuilinda benki hiyo.Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, ulihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.

Akizindua uuzwaji wa hisa hizo, Majaliwa alisema serikali inatambua vilio vya muda mrefu, ambavyo vimekuwa vikitolewa na walimu, hivyo imefarijika na hatua yao ya kuanzisha benki hiyo chini ya chama chao (CWT) bila kutetereshwa na maneno yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya watu kwa lengo la kuwakatisha tamaa. Alisema serikali imejifunza mengi kutoka uanzishwaji wa benki hiyo, hivyo akataka iwe ni chachu ya kudumisha ushirikiano kati yao na walimu.

“Baada ya kupata benki, sasa nunueni hisa ili kupanua mtaji wa benki. Msiruhusu ubadhirifu. Muwe wahamasishaji badala ya kuwa wanaharakati. Serikali itatoa ushirikiano pale mtakapokwama,” alisema Majaliwa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nasama Massinda, alisema iwapo wanachama wote hai 200,000 wa CWT watashiriki katika ununuzi wa hisa, idadi ya washiriki katika uwekezaji wa hisa kupitia masoko ya mitaji nchini unatarajiwa kuongezeka kwa takriban asilimia 100. Alisema CMSA imeweka miongozo ya uuzaji na ununuzi wa hisa njia ya teknolojia ya mawasiliano, ambayo imewezesha kuwapo ununuzi wa hisa kupitia simu za mkononi.

Nchemba alizitahadharisha taasisi, ambazo hazijajiandikisha kulipa kodi kwamba, serikali itatoa maelekezo ili utaratibu unaostahili uchukuliwe iwapo hatua ya kuwashawishi kufanya hivyo itashindikana.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCB, Herman Kessy, alisema CWT inamiliki mtaji wa Sh. bilioni 17, ambao umevuka kiwango cha mtaji wa Sh. bilioni wa kuruhusiwa kuanzisha benki nchini.

Alisema hisa za walimu, ambazo zinatarajiwa kufikia Sh. bilioni 11, zitauzwa kwa njia ya mtandao.Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema Watanzania wana kila sababu ya kujivunia kuwapo kwa benki ya walimu nchini, kwani ni ya kwanza kuanzishwa duniani kote.

CHANZO: NIPASHE

Add a comment (1)

You are here: Home Education news