Hub for education news and events

Wanafunzi 3,076 wakacha kidato cha kwanza Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya, ameagiza kusakwa kwa wanafunzi 3,076 ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari za serikali mkoani hapa mwaka huu.

Machibya alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na wanafunzi hao ambao ni kati ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza baada ya kufaulu mtihani wa taifa wa darasa la saba mwaka jana.

Alisema ametoa agizo hilo kwa maofisa elimu wa shule za sekondari,  bodi za shule  kushirikiana na kamati za maendeleo za kata mkoani hapa kuhakikisha wanawasaka wanafunzi hao, kuwakamata wazazi wao na kuwafikisha mahakamani kwa kushindwa kuwapeka shule.

 Kwa mujibu wa Machibya, Wilaya ya Uvinza inaongoza kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wasioripoti shuleni 732 ambao ni sawa na asilimia 39.48 ya wanafunzi 1, 854 waliochaguliwa katika Wilaya hiyo. 

“Iasikitisha sana watoto wetu ambao tunaishi nao nyumbani mmeshindwa kuwapeleka shuleni kinyume cha sera ya elimu inayomtaka kila mwanafunzi aliyechaguliwa kuripoti shuleni na kuanza masomo hadi kumaliza kidato cha nne, " alisema na kusisitiza kuwa: " Wazazi wote ambao watoto wao waliochaguliwa hawajaripoti shule wahakikishe wanawapeleka shuleni  kabla ya Machi 30 mwaka huu vinginevyo watakamatwa na kufikishwa mahakamani." Aliwataka wakuu wa sekondari kutoa  ushirikiano kwa wazazi kwa kuwapokea wanafunzi waliochaguliwa hata kama hawana  sare ya shule, ada na michango.

ippmedia.com

Powered by Bullraider.com
You are here: Home Education news Wanafunzi 3,076 wakacha kidato cha kwanza Kigoma.