Hub for education news and events

Kenya serikali kutoa huduma ya Internet kwa sekondari 1000

MAMLAKA ya mawasiliano Nchini (CA) inapanga kuweka Intaneti (broadband internet) katika shule 1000 za sekondari za umma nchini kwa gharama ya Sh500 milioni ili kurahisisha masomo kupitia mtandao (online learning). Mradi huo utafaidi shule amabazo zina maabara, kompyuta zinazofanya kazi na vifaa vingine vya teknolojia ya habari (IT).

Akizungumza Jumamosi katika shule ya mseto ya kutwa ya Mulathakari Kaunti ya Meru wakati wa harambee ya kuchangisha pesa ya kujenga ukumbi makuli, Mkurugenzi Mkuu wa CA Bw Francis Wangusi alisema kuwa wanachagua shule ambazo zinaweza kurahisisha mradi huo.


"Tunatumia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutambua shule hizo. Hadi sasa tumetambua shule 894 na tunatarajia kujaza idadi hiyo hivi karibuni, "alisema Bw Wangusi. Aliongeza kuwa shule 1000 zimelipiwa katika mwaka huu wa fedha na baada ya kutambua changamoto wataamua hatua ifuatayo katika mradi huo.

“Tutaamua hatima yam radii huu mwaka ujao kama tutawacha kuweka (Internet) ili kununua kompyuta katika shule hizo kwanza. "Tukianza kuweka kompyuta katika shule zetu tutakuwa na changamoto ya rasilimali na tutalazimika kupunguza idadi ya shule ambazo zitafaidika katika mradi huu kila mwaka wa fedha," alisema.

Umeme shuleni

Aliuliza wadau wa elimu kuhakikisha kuwa shule zote zimewekwa umeme na maabara ya kompyuta ndiposa zifaidike na miradi kama hizo.Bw Wangusi alisema kuwa nchi hii inazaidi ya shule 7,000 za sekondari akiongeza kuwa baadaya ya miaka 10 yote itakuwa na (Internet).

Aliongeza kuwa muunganisho wa Intaneti katika shule zote itasaidia wanafunzi walioko katika maeneo ya mijini na vijijini kupata fursa sawa ya masomo.Mkurugenzi huyo alisema kuwa mamlaka hiyo ina njia mwafaka ya kuwapata wale wanaotumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kueneza chuki au vurugu.

"Vyombo vyetu vya habari lazima yatumike vyema hatutaki watu kujificha nyuma ya uhuru wa kujieleza ili kuzitumia vibaya. "Wale watakaopatikana wakieneza chuki katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii atakabiliwa na sheria," aliongezea.

Chanzo: swahilihub.com

Powered by Bullraider.com
You are here: Home Education news Kenya serikali kutoa huduma ya Internet kwa sekondari 1000