Hub for education news and events

Bajeti elimu ya bure yaongezwa kutoka Bilioni. 18 hadi 22 kwa mwezi

Serikali imeongeza bajeti katika elimu ya bure kutoka Sh bilioni 18 hadi Billioni 22 kwa mwezi, imefanya hivyo ili iweze kutekelezaji wa sera ya elimu bure kwa ngazi ya elimu ya msingi hadi sekondari kidato cha sita.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Elimu ya bure imeanzishwa Januari mwaka jana na serikali ya awamu ya tano ambapo kwa kuanza serikali ilikuwa inatoa Sh. bilioni 18.77 kila mwezi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivi karibumu alikaririwa akisema kuwa serikali inatoa Sh. bilioni 22 kila mwezi kwa ajili ya kuzigawa katika shule zote kutumika kwa shughuli za kiutendaji, Waziri Mkuu alikuwa akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mji mdogo wa Mlowo, Halmashauri ya Mbozi mkoani Songwe. 

Waziri Mkuu alisema kutokana na kutoa kiasi hicho cha fedha, hategemei kusikia walimu wakichangisha wanafunzi michango yoyote kwa ajili ya elimu.

“Tulianza na madawati, tukaja mifumo mashuleni na sasa tumetoa michango, lengo tunataka kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule ahakikishe anasoma bila kubughudhiwa, ikibainika shule yoyote inayotoza, basi watendaji wake ajiandae kutumbuliwa.”

Wananchi waliuliza maswali ambapo Waziri Mkuu alisaidiwa kujibu maswali hayo na wakuu wa idara alijibu kutokana na swali lenyewe, mwisho walifanya tathimini ya ziara ya siku nne ambayo ilimalizika jana.

Powered by Bullraider.com
You are here: Home Education news Bajeti elimu ya bure yaongezwa kutoka Bilioni. 18 hadi 22 kwa mwezi