Hub for education news and events

'Mimi ni Mjinga'

CLEVELAND, Marekani

MWANAMKE mmoja huko Marekani amepewa adhabu ya kubeba bango linalosema kuwa  yeye ni mjinga baada ya kufanya uzembe barabarani na kuhatarisha maisha ya wanafunzi.

Jaji wa mahakama inayosikiliza kesi ya mwanamke huyo (32), amempa adhabu ya kubeba bango hilo kwa muda wa siku mbili kama sehemu ya adhabu yake.

Bango hilo limeandikwa, "Mtu mjinga ndiye anayeweza kupita pembeni ya barabara wakati basi likiwa linawashusha wanafunzi,".

Adhabu nyingine aliyopewa ni leseni yake kushikiliwa kwa muda wa mwezi mmoja na kulipia gharama za mahakama dola 250.

 

Powered by Bullraider.com
You are here: Home Funnynews 'Mimi ni Mjinga'