Hub for education news and events

Watoto darasani

Add a comment (2)

Fanya mtihani

Add a comment (0)

Mwalimu Darasani

Add a comment (0)

We can change

Add a comment (0)

Final Exam

Add a comment (2)

Watoto mafuta

Add a comment (0)

Hali ya madarasa Afrika

Add a comment (0)

Hali ya madarasa Afrika

Add a comment (0)

Kufunga Tai

Add a comment (0)

Maskini wasome wapi

Add a comment (0)

'Mimi ni Mjinga'

CLEVELAND, Marekani

MWANAMKE mmoja huko Marekani amepewa adhabu ya kubeba bango linalosema kuwa  yeye ni mjinga baada ya kufanya uzembe barabarani na kuhatarisha maisha ya wanafunzi.

Jaji wa mahakama inayosikiliza kesi ya mwanamke huyo (32), amempa adhabu ya kubeba bango hilo kwa muda wa siku mbili kama sehemu ya adhabu yake.

Bango hilo limeandikwa, "Mtu mjinga ndiye anayeweza kupita pembeni ya barabara wakati basi likiwa linawashusha wanafunzi,".

Adhabu nyingine aliyopewa ni leseni yake kushikiliwa kwa muda wa mwezi mmoja na kulipia gharama za mahakama dola 250.

 

Add a comment (1)

East africa class

Add a comment (0)

Doing Exam

Add a comment (0)

Watoto wakila

Add a comment (0)

Darasa Kampala

Add a comment (0)

Wakati wa kuchemsha bongo

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


Chemsha bongo.

Add a comment (0)

Elimu na vichekesho

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 Kama mbwa wanasoma sisi binadamu tushwindwe nini?

Add a comment (1)

Mwalimu na burudani

Mwalimu mbali na kufundisha mambo mengine pia alifundisha burudani.

Add a comment (0)

Umeweza nini leo

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tafakari .....

Add a comment (0)

Darasa chini ya mbuyu

Hali halisi ya elimu Afrika Mashariki

Add a comment (0)

Wanafunzi Darasani

Add a comment (0)

TZ kuingizwa Guinness

 

KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema Tanzania inastahili kuingia katika kitabu cha kumbukumbu cha Maajabu ya Dunia cha The Guinness Book of Records kwa kufaulisha wanafunzi 5,200 wasiojua kusoma wala kuandika.

Akiwasilisha maoni ya upinzani bungeni, Msemaji mkuu kuhusu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo alisema hiyo ni kashfa kubwa kwa Serikali ya CCM. “Hii ni kashfa kubwa na kama kweli Serikali hii ingekuwa inafuata misingi ya utawala bora na uwajibikaji, basi leo viongozi wakuu wa elimu wangeshaachia ngazi, lakini tumeendelea na utamaduni wa kufanya mambo kwa mazoea,” alisema.

Kambi hiyo ilidai inashangaa mpaka sasa Waziri na Naibu wake wapo madarakani wakishangilia ushindi wa kuongoza taifa kushika nafasi ya kwanza duniani kwa kufaulisha wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.

“Kambi rasmi ya upinzani inahoji hivi ni mpaka Waziri Mkuu atishiwekupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, ndiyo Waziri wa Elimu na Naibu wake wajiuzulu?... kwanini wasiwajibike kwa uzembe na makosa ya waziwazi?” ilihoji.

Lyimo alisema tatizo la wanafunzi kuhitimu elimu ya msingi bila kujua kusoma wala kuandika, ni ufisadi wa aina yake katika sekta ya elimu, watendaji hawatimizi wajibu wao ipasavyo na wanajihusisha na vitendo vya rushwa. Vitendo hivyo vya rushwa vinadaiwa kusababisha kuvuja kwa mitihani, hivyo kuwalemaza wanafunzi kifikra kwa kuwaaminisha kwamba kufaulu

kunawezekana bila bidii katika masomo.  Mwaka jana wanafunzi 9,736 walifutiwa matokeo.

“Huu ni ushahidi tosha kuwa sekta ya elimu kuna mafisadi wenye uchu wa utajiri wa harakahara kwa gharama yoyote ikiwamo kuiua elimu yetu kwa kuuza mitihani,” alisisitiza Lyimo katika hotuba

yake hiyo.

Lyimo aliwaangukia walimu nchini akiwaomba wasaidie kuwaelimisha Watanzania juu ya umuhimu wa kufanya mabadiliko ya uongozi kwa maslahi ya nchi na mustakabali mzima wa maendeleo ya elimu.

Halikadhalika kambi hiyo imeionya Serikali isifikiri kutokuwapo kwa mgomo halisi (Active Strike) ndiyo imemaliza tatizo la madai ya walimu, kwani kuna migomo baridi inayoendelea kwa baadhi ya walimu.

“Athari za migomo baridi huwa ni mbaya zaidi ya mgomo halisi kama walimu wataamua kulipiza kisasi kwa kuwafundisha watoto vitu visivyo halisi, basi kuna hatari kubwa ya kupata kizazi kisicho na elimu kabisa”alisisitiza Lyimo.

Kauli hiyo ya kuporomoka kwa elimu nchini, iliungwa mkono pia na Mbunge wa Viti Maalumu, Maulida Komu (Chadema) wakati akichangia bajeti hiyo.

Mwananchi.co.tz

Add a comment (0)

You are here: Home Fanny::Blog