Hub for education news and events

Apple watoa iBulb

KUTOKA kwa kampuni kubwa kama Apple tegemea maajabu yoyote, kwa wanafunzi wanasubiri kwa hamu siku kampuni hiyo itakapogundua app inayoweza kuandika notes kwenye madaftari.Lakini sasa baada ya kugundua, iMac, iPad, iPod, iPhone na vitu vingine vingi, sasa wamekuja na iBulb taa ambayo unaweza kuibadilisha rangi kadri upendavyo kwa kutumia app ambayo ipo kwenye simu za iPhone na iPad. Taa hiyo ambayo inazwa paundi 45, unaweza kuizima na kuiwasha muda wowote, ukiwa mahali popote duniani ilimradi tu uwe na simu za aina hiyo.

Apple wanasema wametengeneza taa hiyo ili kuwarahisishia kazi wateja wao ambao mara nyingi wanakuwa mbali na nyumbani muda ambao wanatakiwa kuwasha taa.

Aidha wamesema  wamewezesha kubadilisha rangi ili mtu anapokuwa mbali na nyumbani kwake abadilishe kila mara kuwatisha wezi ambao wataamini ndani ya nyumba kuna mtu.

Lakini si tu wanalenga wateja wao wawapo mbali na majumbani, hata waliopo nyumbani wakati mwingine mtu anaona uvivu kuinuka kuwasha au kuzima taa, kwa maana hiyo anachohitaji karibu yake ni simu tu.

Taa hizo zimetengenezwa na kampuni maarufu ya Kidachi, Philips. Huchomekwa katika socket za kawaida za taa isipokuwa tu huja na kifaa maalum ambacho huunganishwa katika simu ya mwenye nyumba.

Powered by Bullraider.com
You are here: Home Technology news Apple watoa iBulb