Hub for education news and events

Ubao, madaftari na chaki vitabaki Bongo


MADARASA ambayo yatakuwa na kila kitu katika mfumo wa 'touchscreen' ndio habari inayotaka kuuteka ulimwengu sasa. 

 

Kwa maana hiyo baada ya muda mchache tutakaobaki kutumia ubao, chaki na madaftari vitabaki kwetu sie ambao teknolojia inachelewa kutufikia.

Utafiti ulifanyika kwa miaka minne umeweza kuvumbua  kitu mfano wa meza kubwa ambacho ni 'touchscreen'.Kifaa hiki kinaweza kutumika kwa walimu kufundishia na wanafunzi kusomea na kuandika.

Watafiti hao kutoka Durham Univesity wamegundua kitu hiki kinachoitwa 'Star Trek classroom' au 'classroom of the future' ambacho hakitawafanya waalimu washike chaki tena wala wanafunzi wabebe madaftari.

Watafiti hao wamesema pia ugunduzi huo umeonyesha kuwasaidia wanafunzi, katika kuwa na uwezo zaidi katika hesabu tofauti na katika mfumo wa kuandika kwenye madaftari.

Aidha wanasema dawati hilo linawafanya wanafunzi wafanye kazi kwa pamoja, kitu ambacho kinaongeza juhudi kwa hata yule aliyekuwa na tabia ya kutegea.

Mtafiti Mkuu, Profesa Liz Burd anasema hata wakati wanatengeneza lengo lao kubwa lilikuwa ni kuona wanafunzi wanashiriki moja kwa moja darasani.

Dawati hilo linaweza kutumiwa na wanafunzi wawili mpaka watatu, mwalimu anaweza kuwatumia kazi kutoka dawati jingine.

Powered by Bullraider.com
You are here: Home Technology news Ubao, madaftari na chaki vitabaki Bongo