Hub for education news and events

Umejiaadaa kwa simu za kukunja?

OK! Jiandae kwa simu ya mkononi ambaye inaweza kukunjwa na kukunjuliwa kadri upendavyo na kuitupia ndani ya waleti yake yenye ukubwa wowote. Baada ya kutengeneza kila aina ya 'gadget', Samsung inajiandaa kutengeneza simu mpya ambazo zinakunjika; bila shaka hizi zitakuwa hazivunjiki kwasababu lazima zitakuwa za mpira.Kampuni inayotengeneza simu za aina hii ambayo makao makuu yake yapo nchini Korea imesema kuwa, utengenezaji wa simu hizi uko katika hatua za mwisho na mapema mwakani zitaingia sokoni.

Utengenezaje wa simu hizo umefanikiwa baada ya kuanza kwa kutumika kwa kifaa kiitwacho (OLEDs) ambacho ni muhimili mkuu katika kuiwezesha simu bila kutegemea vyuma na madini mengine magumu.

Kwa kutumia OLEDS samsung inaweza kutengeneza simu kwa plastic au karatasi ya foil. Wenyewe wanasema wametengeneza simu hiyo ili kuweza kutofautisha kwa kuwa sasa hivi wateja wanashindwa kuchagua kutokana na ukweli kwamba, karibu kila aina ya simu ya kampuni moja infanana na nyingine.

Lakini wanasema kuwa simu hizi pia zitakuwa imara na nyepesi kuliko simu zote zilizowahi kutokea duniani.

Powered by Bullraider.com
You are here: Home Technology news Umejiaadaa kwa simu za kukunja?