Hub for education news and events

Ijue ‘selfie stick’

Kwa wafuatiliaji wa masuala ya teknolojia ‘selfie stick’ sio msamiati mgeni masikioni mwao, lakini kwa faida ya wengine hiki ni kifaa ambacho hutumika kushikilia simu au kamera ndogo wakati wa kujipiga picha kama kinavyoonekana pichani.


Jina lake linasawiri umbo wa kifaa hiki ambacho ni chuma kilicho katika muundo wa fimbo ndefu chenye mshikio hivyo kumuwezesha mtumiaji kushika kwa urahisi wakati wa kupiga picha.

Selfie stick inakuwa na kitako ambacho hutumika kuwekea simu. Baada ya kushikizwa kwenye kitako simu inaunganishwa na kijiti hicho cha kielektroniki tayari kwa zoezi la kupiga picha. Kijiti hiki kinakuwa na kitufe maalum ambacho kinaunganisha mawasiliano kati yake na simu. Unapokuwa tayari kupiga unaelekeza kamera eneo lilipo na kukibonyeza kitufe hicho.

Kifaa hiki kimekuwepo kwa muda mrefu katika nchi zilizoendelea lakini huku kwetu umaarufu wake umeanza kuonekana mwaka juzi. Umaarufu wa selfie stick umekuja katika kipindi ambacho mtandao wa Instagram unaohusisha uwekaji wa picha ukiwa umeshika kasi.

Wakati Tanzania na mataifa mengine ya Afrika wakiendelea kujifunza kutumia kifaa hiki, nchi nyingi za Ulaya zimepiga marufuku matumizi yake ikiwamo Australia.
Selfie stick imepigwa marufuku katika viwanja vikubwa vya mpira duniani ukiwemo wa Emirates unaomilikiwa na klabu ya Arsenal.

Sababu kubwa ya kupigwa marufuku selfie stick ni kile kinachodaiwa kuleta usumbufu kwa watu wengine wakati mhusika anahangaika kujipiga picha.
Idadi kubwa ya watu wanaopata madhara hata kufikia kupoteza maisha  wakati wakipiga picha za mtindo huu ni sababu nyingine iliyochangia selfie stick kupigwa marufuku katika baadhi ya maeneo.

Powered by Bullraider.com
You are here: Home Technology news Ijue ‘selfie stick’