Hub for education news and events

Unaigusa simu yako mara 2,617 kwa siku

Takribani karne moja sasa binadamu wamekuwa ‘wakiitembelea’ dunia kupitia  simu za mkononi iwe kwa kupigiana au kutumiana ujumbe mfupi wa maandishi au kuwasiliana katika mitandao ya kijamii.

Kutokana na kukua kwa teknolojia, mawasiliano yamekuwa bora. Sasa unaweza kuzungumza na mtu kwa kutuma ujumbe, kupiga simu za kawaida au za video popote pale duniani.
Mawasiliano yamewaweka watu karibu lakini kukua kwa teknolojia kumekifanya kifaa hiki kuwa na umuhimu wa kipekee kwa binadamu.
 
Hali hii imewafanya wengine kuwa ‘watumwa’ au ‘wagonjwa’ wa kifaa hiki cha mawasiliano. Siku huwa ngumu na ndefu unapokikosa.Hebu fikiri unavyojisikia pale simu yako inapokwisha chaji. Au maumivu unayoyapata unapoipoteza au kuiharibu.

Simu ni sehemu ya maisha ndiyo maana utakapoishiwa chaji utahaha kuisaka mpaka uipate na pale inapoharibika au kupotea utaharibu bajeti zako ununue mpya.

Wanasayansi wamefanya utafiti kwa kuwaangalia watumiaji wa simu 94 ili kujua ni mara ngapi kwa siku huwa wanazigusa. Utafiti huo umegundua kuwa kwa siku moja mtu huyu huiangalia na kuigusa simu yake mara 2,617 kwa siku.

Apple watoa iBulb

Kwa hesabu hizi mtu mmoja huigusa simu yake mara milioni moja. Inaweza kuonekana kuwa mara milioni moja kwa mwaka ni nyingi sana, lakini wapo wanaozigusa mara mbili ya hawa.

Powered by Bullraider.com
You are here: Home Technology news Unaigusa simu yako mara 2,617 kwa siku